• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatetea kuunga mkono kanda ya Afrika ya Kati kukabiliana na matishio kwa msingi wa kuheshimu haki za uongozi za Afrika

    (GMT+08:00) 2018-12-15 17:06:03

    Naibu balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao juzi aliitaka jumuiya ya kimataifa iunge mkono nchi za kanda ya Afrika ya Kati kukabiliana na matishio kwa msingi wa kuheshimu haki za uongozi za Afrika, na kuzisaidia nchi hizo kutimiza lengo la usalama na utulivu na kuendeleza uchumi.

    Bw. Wu alisema hayo wakati Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilipokagua na kujadili hali ya kanda ya Afrika ya Kati na suala la kundi la Lord's Resistance Army. Amesema hivi karibuni mchakato wa kisiasa wa nchi za kanda ya Afrika ya Kati umekuwa ukipata maendeleo, lakini nchi hizo bado zinakabiliwa na matishio ya makundi ya kigaidi, na jumuiya ya kimataifa inapaswa kuongeza nguvu ya kuzisaidia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako