• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yashindwa kujibu pendekezo Russia kujadili mkataba wa INF

    (GMT+08:00) 2018-12-15 17:09:49

    Russia imesema waziri wake wa Ulinzi Bw. Sergei Shoigu hajapokea jibu lolote kutoka kwa Marekani kuhusu kujadili maoni yao tofauti kuhusu mkataba wa makombora ya nyuklia ya masafa ya kati, kati ya nchi hizo mbili INF.

    Pendekezo hilo ni moja ya mapendekezo mawili yaliyotumwa na Bw. Shoigu kwa waziri wa ulinzi wa Marekani Bw. James Mattis, pendekezo lingine ni kuhusu suala la Syria. Taarifa ya wizara ya ulinzi ya Russia imesema Russia iko tayari kufanya mazungumzo na wizara ya ulinzi ya Marekani kuhusu mambo yote muhimu. Lakini siku tatu baada ya ujumbe wa Russia kupokelewa, wizara ya ulinzi ya Russia haijapata majibu yoyote kutoka kwa Marekani.

    Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema kukaa kimya kwa Marekani, kunaonyesha kuwa Marekani haiko tayari kufanya mazungumzo na Russia kutatua maswala ya usalama ya kikanda na dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako