• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakanusha kauli ya ofisa wa Marekani kukosoa uhusiano kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-12-15 17:13:36

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amepiga kauli iliyotolewa na mshauri wa mambo ya usalama wa Marekani Bw. John Bolton, akikosoa ushirikiano wa kibiashara wa China na Russia na nchi za Afrika, kuwa unadumaza ongezeko la uchumi wa Afrika , unatishia uhuru wa kifedha wa nchi za Afrika, unazuia fursa za uwekezaji wa Marekani barani Afrika, unaingilia operesheni za kijeshi za Marekani na kuwa tishio kwa usalama wa Marekani.

    Akikosoa shutuma hizo, Bw. Kang amesema inachojali China ni mahitaji ya nchi za Afrika , kama vile maendeleo ya viwanda na kuboresha kilimo. Ametolea mifano ya mkutano wa Beijing wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCA uliofanyika mwaka huu, na Mkutano mkuu wa 73 wa umoja wa mataifa, ambapo viongozi wengi wa nchi za Afrika walipongeza uungaji mkono wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako