• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazindua kampeni ya usalama wa chakula katika maeneo ya vijijini

    (GMT+08:00) 2018-12-16 16:47:52

    Mamlaka za China, ikiwemo wizara ya kilimo na mambo ya vijijini, imezindua kampeni ya nchi nzima ili kutafuta bidhaa za chakula zilizo feki na zisizofikia kiwango katika maeneo ya vijijini.

    Kampeni hiyo inalenga kukabiliana kwa ufanisi na makosa makubwa ya aina sita kabla ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, itakayokuwa Februari 5, 2019. Vyombo vya sheria vitalenga vyakula vya haraka, vitafunio, pombe, bidhaa zinazoongeza ladha ya chakula pamoja na bidhaa zinazotokana na maziwa na nyama. Wakati huo huo bidhaa zinazotumiwa kwa wingi vijijini, ambazo zimewekewa taarifa za uwongo na ambazo hazijafikia viwango pia zitashughulikiwa kwenye kampeni hiyo. Waziri wa kilimo na mambo ya vijijini Han Changfu amesema wale wote wanaohusika na makosa hayo watafungiwa na kupelekwa polisi kama itahitajika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako