• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakabiliana na matatizo na changamoto kwa hatua zenye busara

    (GMT+08:00) 2018-12-17 17:04:10

    Mkutano wa tatu wa Kamati kuu ya awamu ya 11 ya Chama cha kikomunisti cha China uliofanyika kuanzia tarehe 18 hadi 22 mwaka 1978, unachukuliwa kama mwanzo wa utekelezaji wa sera za mageuzi na ufunguaji mlango wa China. Katika miaka 40 iliyopita, mfumo wa ujamaa wa China unaolenga kukomboa na kuendeleza uwezo wa uzalishaji wa jamii, kuiendeleza China ulikundwa, wakati huo huo umehakikisha sera mbalimbali zinazosaidia chama cha kikomunisti cha China kujiendeleza zinapata mafanikio kuwasaidia watu zaidi ya milioni 700 kuondokana na umaskini, na kuifanya China kuwa nchi ya pili kwa nguvu ya uchumi. Uzoefu wa kujiendeleza wa China umepongezwa na nchi nyingi duniani, na hatua zenye busara za China zimechangia kutatua matatizo kadhaa yanayoikabili dunia kwa hivi sasa.

    Mwaka 1978 wakati sera ya mageuzi na ufunguaji mlango ilipoanza kutekelezwa nchini China, mfumo wa uchumi unaopangwa na serikali ulikuwa unakwamisha maendeleo ya uchumi na uvumbuzi wa kijamii. Mkuu wa Bodi wa Kampuni ya Asiatique ya Ufaransa ambaye pia naibu mwenyekiti wa Kamati ya Ufaransa na China Bw. Qian Faren ni mchina aliyezaliwa nchini Ufaransa, anasema:

    "Nilipoenda China kufanya kazi, niliona kuwa kuna pengo kubwa kati ya China na nchi za magharibi, kwa mfano tukitaka kununua vitu tulipaswa kutumia pesa pamoja na kuponi za chakula, vitambaa…"

    Lakini baada ya kutekeleza sera mbalimbali za mageuzi na ufunguaji mlango katika sekta mbalimbali, hivi sasa China imekuwa nchi ya pili kwa nguvu ya uchumi duniani, thamani ya jumla ya uzalishaji wa ndani imekuwa dola za kimarekani trilioni 11.99, pato la wastani limefikia dola za kimarekani elfu 8.7. Waziri mkuu wa zamani wa Ufaransa Bw. Dominique de Villepin anaona kuwa mafanikio hayo ya China yanahusiana na ufanisi na ushirikiano. Anasema:

    "Katika miaka 40 iliyopita, China imepata mabadiliko makubwa katika sekta za uchumi, jamii na uongozi duniani. Mafanikio hayo hayakupatikana kwa bahati, bali yanatokana na mipango ya muda mrefu na yenye ufanisi. Aidha ufunguaji mlango na ushirikiano pia una umuhimu mkubwa."

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe anaona kuwa Zimbabwe inahitaji mwenzi kama China kuisaidia kuhimiza maendeleo, kuimarisha na kukuza ushirikiano wenye ufanisi, kutafiti uzoefu wa China katika mageuzi na ufunguaji mlango katika miaka 40 iliyopita. Anasema:

    "Uchumi wa China umepata maendeleo kwa kasi, huku jamii na utamaduni pia vikipata maendeleo makubwa. Zimbabwe inatakiwa kujifunza kutoka kwa China, na kupata uzoefu muhimu wa kupata njia ya maendeleo inayolingana na hali yake yenyewe."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako