• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kujenga na kukarabati vyoo 21,000 kwa ajili ya utalii mwaka 2019

    (GMT+08:00) 2018-12-17 18:16:05

    China inatarajia kujenga na kukarabati zaidi ya vyoo 21,000 katika maeneo ya utalii hadi kufikia mwakani ikiwa ni sehemu moja ya mpango ulioanza mwaka 2015 wenye lengo la kuwa na vyoo vya kisasa kwa watalii.

    Hayo yametangazwa na Wizara ya utamaduni na utalii ya China katika Mkutano wa wadau wa watalii uliofanyika katika mkoa wa Guangdong, kusini mwa China mwishoni mwa wikiendi iliyopita.

    Wizara hiyo imebainisha kuwa, mwaka huu imekwishajenga jumla ya vyoo 24,000 kwa ajili watalii, vikiwa ni pamoja na 15,000 katika maeneo yaliyoko nyuma kiuchumi.

    Tokea mwaka 2015 hadi 2017, China imewekeza yuan bilioni 1.64, sawa na dola za Marekani milioni 237.8 kwa ajili ya mradi huu ambao utasaidia kukuza utalii wa ndani kulingana na mpango wa serikali wa kukuza utalii kwa miaka mitatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako