• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Fastjet yapewa siku 13 kufanya marekebisho

  (GMT+08:00) 2018-12-17 19:35:29

  Shirika la ndege la Fastjet Tanzania limepewa siku 13 kufanya marekebisho ya utendaji au lifutiwe leseni.

  Siku za hivi karibuni shirika hilo ambalo linajinasibu kwa kutoa usafiri wa gharama nafuu limegubikwa na matukio ya kuahirisha safari zake, jambo ambalo limesababisha Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) kusitisha safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda Zambia na Zimbabwe.

  Kufuatia hatua hiyo, Desemba 14, shirika hilo liliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa twitter likieleza kusitishwa kwa safari hizo hadi hapo zitakapotangazwa tena.

  Mkurugenzi mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema shirika hilo lilipewa siku 28 za kufanya marekebisho ya utendaji wake tangu Desemba 2.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako