• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raga- Afrika Kusini kuvaana na wenyeji Japan katika mchezo wa kirafiki wa raga kuelekea Kombe la dunia mwaka 2019

    (GMT+08:00) 2018-12-18 09:44:26

    Afrika Kusini itavaana na wenyeji Japan katika mchezo wa kirafiki wa raga ikiwa kwenye harakati za kujiandaa na Kombe la dunia mwaka 2019. Japan ilisababisha maafa makubwa kwa Afrika Kusini katika historia ya kombe la dunia baada ya kuichabanga 34-32 nchini Uingereza miaka mitatu iliyopita. Kocha wa Springboks ya Afrika Kusini Rassie Erasmus amesema hii ni fursa nzuri ya kujiandaa na mechi za kombe la dunia. Springboks watazikabili Australia, New Zealand na Argentina kwenye michuano ya mabingwa ya raga kabla ya kusafiri kuelekea Japan.

    Afrika Kusini ipo nafasi ya 5 duniani na inachukuliwa kama miongoni mwa nchi zinaweza kuifunga bingwa mtetezi New Zealand katika kombe la dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako