• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatangaza "Alama ya Siri ya Mafanikio" ya hatua ya mageuzi na ufunguaji mlango

    (GMT+08:00) 2018-12-18 17:09:46
    Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba muhimu kwenye Mkutano wa Maadhimisho ya miaka 40 ya sera ya mageuzi na ufunguaji mlango uliofanyika leo, akijumuisha hatua, mafanikio, umuhimu na uzoefu muhimu zilizopatikana na China katika hatua ya utekelezaji wa mageuzi na ufunguaji mlango katika miaka 40 iliyopita, na pia ametangaza maagizo ya kuwahamasisha wanachama wa Chama cha kikomunisti cha China na wananchi wote kuendelea kusukuma mbele hatua hiyo katika zama mpya.

    Hotuba aliyoitoa rais Xi imejumuisha mafanikio yaliyopatikana katika hatua ya utekelezaji wa sera ya mageuzi na ufunguaji mlango katika miaka 40 iliyopita, ambayo yanahusisha nyanja kumi zikiwemo mawazo na nadharia, ujenzi wa uchumi, mambo ya siasa ya kidemokrasia, maendeleo ya utamaduni, uboreshaji wa maisha ya wananchi, ulinzi wa hali ya ikolojia, mambo ya kisasa ya ulinzi wa taifa na ujenzi wa jeshi, muungano wa amani, mambo ya diplomasia ya amani, na ujenzi wa chama. Rais Xi amesisitiza kuwa mageuzi na ufunguaji mlango yamebadilisha sana sura ya nchi, taifa la China, wananchi pamoja na chama cha kikomunisti cha China, ambapo dunia si kama tu inaweza kupata "Alama ya Siri ya Mafanikio" katika hatua hiyo ya China, bali pia inaweza kujua kwa nini viongozi na wananchi wa China wana nia na imani ya kutekeleza kihalisi sera hiyo.

    Rais Xi amesema uzoefu muhimu uliopatikana katika hatua hiyo ni pamoja na kushikilia umuhimu wa kuimarisha na kuboresha uongozi wa chama, kutoa kipaumbele malshi ya wananchi, kuendeleza ujamaa wenye umaalum wa kichina, kuweka kipaumbele katika maendeleo, kupanua ufunguaji mlango, na kushughulikia mambo ya chama kwa nidhamu kali.

    Katika miaka 40 iliyopita, China imekuwa nchi ya pili yenye nguvu ya uchumi duniani kutoka nchi ambayo uchumi ulikaribia kuvunjika; pia imepunguza idadi ya watu maskini kwa watu milioni 740, na wastani wa pato la wakazi wote umefikia dola elfu 3.8 za kimarekani. Wakati huo huo imekuwa mjenzi anayekubalika na jumuiya ya kimataifa wa dunia ya amani, mchangiaji wa maendeleo ya dunia, na mlinzi wa utaratibu wa kimataifa… Rais Xi akizungumzia hayo alisema kwa fahari kubwa kwamba, China imemaliza mchakato wa maendeleo ya viwanda kwa miaka miongo kadhaa ambao nchi zilizoendelea zilitumia karne kadhaa. Mambo yasiyowezekana yametimizwa na wananchi wa China.

    Hivi sasa hatua ya China ya mageuzi na ufunguaji mlango inakabiliwa na mwanzo mpya wa kihistoria: Mkutano mkuu wa 19 wa Kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China umeweka mkakati wa kuijenga China kuwa jamii yenye maisha bora hadi kutimiza kimsingi mambo ya kisasa, na kujenga kwa pande zote nchi yenye nguvu ya mambo ya kisasa ya ujamaa. Wakati huo huo hali ya kujilinda kibiashara na utaratibu wa upande mmoja unafufuka, huku mafungamano ya kiuchumi yakikwama, na hali ya kutotabirika inaongezeka. Ili kukabiliana na changamoto hizo, China itaendelea kutimiza kihalisi ubashiri wa mshindi wa tuzo ya somo la uchumi ya Nobel Bw. Ronald H. Caose, na kuleta mafanikio makubwa zaidi kwa China inayofungua mlango, yenye uvumilivu, imani kubwa na uvumbuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako