• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuinua uwezo na kiwango cha umaalumu wa mashirika

    (GMT+08:00) 2018-12-18 19:35:28

    Naibu waziri wa viwanda na teknolojia ya habari wa China Bw. Wang Jiangping hapa Beijing amesema, China itayaongoza mashirika kushikilia njia ya kuendeleza umaalumu, kuinua uwezo na kiwango cha umaalumu wa mashirika, ili kuhimiza maendeleo ya kiwango cha juu ya utengenezaji wa bidhaa.

    Bw. Wang amesema, ili kuhimiza maendeleo ya umaalumu kuna umuhimu mkubwa katika maendeleo ya kiwango cha juu ya utengenezaji wa China. Pia amesema, shughuli ya utengenezaji wa bidhaa ya China ina upungufu wa uwezo wa uvumbuzi, tatizo la kiwango cha chini cha maendeleo. Kwa kulinganishwa na kiwango cha juu cha kimataifa, utengenezaji wa bidhaa wa China bado una upungufu mkubwa katika sekta nyingi.

    Ameongeza kuwa ili kutatua matatizo hayo na kuhimiza maendeleo ya shughuli ya utengenezaji wa bidhaa, China itakuza mashirika bora hasa mashirika yanayoongoza katika sekta mbalimbali. Hivi sasa,China imechagua makundi matatu ya mashirika bingwa katika utengenezaji wa bidhaa kwa nyakati tofauti, ambayo ujumla wa mashirika 390 umeorodheshwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako