• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China atoa hotuba muhimu katika Mkutano wa Maadhimisho ya miaka 40 ya sera ya mageuzi na ufunguaji mlango

    (GMT+08:00) 2018-12-18 21:00:45
    Mkutano wa Maadhimisho ya miaka 40 ya sera ya mageuzi na ufunguaji mlango umefanyika leo hapa Beijing. Rais Xi Jinping wa China akihutubia mkutano huo amesisitiza kuwa maendeleo ya China yametoa uzoefu mzuri wa kupata mafanikio kwa nchi mbalimbali zinazoendelea duniani kupiga hatua ya mambo ya kisasa, ambao pia umetoa msukumo mkubwa kwa kuhimiza amani na maendeleo ya dunia. Pia amesisitiza kuwa mageuzi na ufunguaji mlango ni uzoefu muhimu kwa Chama na wananchi wa China kujiendeleza kwa kufuata mkondo wa wakati, pia ni njia ya lazima kwa kushikilia na kukuza ujamaa wenye umaalumu wa kichina, vilevile yana umuhimu mkubwa katika kutimiza ustawi wa taifa la China.

    Rais Xi Jinping amesema China inapaswa kuendelea kutoa kipaumbele katika maendeleo, ili kuongeza nguvu ya taifa, kushughulikia vizuri pengo kati ya mahitaji ya maisha bora ya wananchi na hali ya kutokuwepo kwa maendeleo yenye uwiano na ya kutosha, kubadilisha njia ya maendeleo kwa hatua madhubuti na kuboresha muundo wa uchumi, kutekeleza mkakati wa kuhimiza maendeleo kupitia uvumbuzi, na kuimarisha ujenzi wa mazingira.

    Rais Xi Jinping amesema, sera ya mageuzi na kufungua mlango inapaswa kuzingitia zaidi mambo ya wananchi, na kuendana na matumaini yao, kuheshimu maoni yao, kufuatilia hali zao, na kushugulika na kazi za kuboresha maisha yao.

    Rais Xi Jinping amesema China haiwezi kupata maendeleo kama ikijitenga na dunia, na ustawi wa dunia pia hauwezi kupatikana bila China. China inapaswa kushikilia kufungua mlango zaidi, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya yenye mustakbali wa pamoja. Amesema, China itahimiza kujenga uhusiano mpya wa kimataifa wenye haki na usawa na wa kuheshimiana, kushirikiana ili kupata mafanikio ya pamoja, kuheshimu haki ya watu wa nchi nyingine ya kuchagua njia ya kujiendeleza, kusaidia nchi zinazoendelea kupata maendeleo, kuunga mkono utaratibu wa biashara wa pande nyingi, na kuanzisha majukwaa mapya ya kimataifa ya ushirikiano haswa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Rais Xi Jinping amesema China inapaswa kushughulikia vizuri uhusiano kati ya mageuzi, maendeleo na utulivu, na China ni nchi kubwa ambayo haitakiwi kufanya makosa makubwa katika masuala kuu. Ameagiza kuhakikisha hatua kubwa za mageuzi zinatekelezwa kihalisi, na kuunganisha juhudi za kuhimiza mageuzi, maendeleo na utulivu.

    Rais Xi Jinping amesema China inapaswa kushughulikia vizuri uhusiano kati ya mageuzi, maendeleo na utulivu, na China ni nchi kubwa ambayo haitakiwi kufanya makosa makubwa katika masuala kuu. Ameagiza kuhakikisha hatua kubwa za mageuzi zinatekelezwa kihalisi, na kuunganisha juhudi za kuhimiza mageuzi, maendeleo na utulivu.

    Kwenye mkutano huo Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na baraza la serikali la China zimetoa tuzo ya urafiki ya mageuzi ya China kwa wageni 10, ili kuwashukuru kwa mchango wao wa kuhimiza mawasiliano na ushirikiano kati ya China na nchi za nje, na kushiriki na kuunga mkono mchakato wa mageuzi na kufungua mlango nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako