• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Riadha: AK kusajili makocha Januari mwakani

    (GMT+08:00) 2018-12-19 09:15:36

    Shirikisho la Riadha nchini Kenya AK limetanganza kuwa makocha wote wanaotaka kufanya kazi nchini huko mwaka 2019 watalazimika kujisajili katika ofisi zake za Riadha House January 9. Kwenye taarifa yake AK imesema wamewataka wenyeji na wageni waishio na kufanya kazi Kenya kuwasilisha vibali vyao vya kuishi na vyeti vya ofisi zao. Shirikisho hilo limesema zoezi hilo linalenga kuhakikisha makocha wote wanaofanya kazi nchini humo wana sifa ya kuwafunza wanariadha. Na kwa makocha wote ambao hawatakuwepo nchini watapewa nafasi nyiongine ya kuwasilisha nyaraka zao baadaye. AK imesisitiza kuwa wale wanaoshindwa kuwasilisha nyaraka zao watalilazimisha shirikisho kuongea na mashirika mengine ya serikali ili wachukuliwe hatua za kisheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako