• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bidhaa za mazao ya kilimo za Kenya zalengwa kwa soko la China

    (GMT+08:00) 2018-12-19 17:01:22

    Maonesho ya kwanza ya kimataifa ya uingizaji wa bidhaa ya China CIIE yalimalizika mwezi mmoja uliopita, lakini bado yanaonesha umuhimu mkubwa kwa nchi nyingi ikiwemo Kenya. Makubaliano yaliyofikiwa kwenye maonesho hayo yamezihimiza kampuni za Kenya kuingia kwenye njia ya mwendo wa kasi ya kuuza bidhaa nchini China, na bidhaa nyingi za mazao ya kilimo za Kenya ikiwemo maua, mkahawa, chai, maparachichi na maembe zinalengwa na soko la China.

    Bw. He Qinwen anayeshughulikia uuzaji wa bidhaa nchini Kenya, alikuwa mratibu wakati wa Mkutano wa CIIE akishughulikia mambo ya kuisaidia serikali ya Kenya kujenga banda lake kwenye maonesho hayo. Hadi sasa anapenda kuzungumzia mambo mbalimbali yaliyotokea kwenye jumba hilo. Wakati wa maonesho hayo, banda la Kenya lilikuwa moja ya mabanda yaliyofurahisha zaidi watu. Anasema:

    "Kwa nini banda la Kenya liliwavutia watu wengi? Kila siku jumba hilo lilikuwa linajaa watu. Wengi walisema wanataka kuonja kahawa na chai ya Kenya. Mbali na hayo maua yaliyosafirishwa kutoka Kenya yalikuwa mengi sana kwenye jumba hilo, pia kulikuwa na vitu vingi vya sanaa vyenye mtindo wa Kenya."

    Uchumi wa Kenya unategemea zaidi kilimo na utalii, mbali na hayo uuzaji wa chai katika nchi za kigeni pia unashika nafasi mbili za mwanzo duniani, wakati huo huo uuzaji wa maua kutoka nchi hiyo katika nchi za nje ni mkubwa. Katika miaka ya hivi karibuni, China imekuwa soko linalokua kwa kasi zaidi kwa uuzaji wa maua wa Kenya. Wakati huo huo bidhaa nyingine za mazao zikiwemo maharage, maparachichi na maembe pia zinatarajiwa kulengwa katika soko la China.

    Mwanzilishi wa Kampuni ya chai ya Kenya Home Comforts LTD aliyeshiriki kwenye Maonesho ya CIIE Bw. Brian Mchiri, siku zote ana imani kubwa juu ya soko la China. Kwa maoni yake, Maonesho ya CIIE yametoa fursa nzuri kwa wakenya kushuhudia soko la China lenye uhai mkubwa, na kufahamu mahitaji ya wateja wa China. Anasema:

    "Tumewasiliana na majukwaa mbalimbali ya biashara ya kielektroniki, pamoja na wateja wa rejareja, ambayo ni fursa nzuri tuliyopewa na maonesho hayo. Hivi sasa tumetathmini fursa mbalimbali za kibiashara, na tutawasiliana na wenzi wa ushirikiano katika siku zijazo, ikiwa ni sehemu ya fursa mbalimbali za kibiashara."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako