• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito wa msaada wa kimataifa kusaidia amani Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2018-12-19 18:17:28

    Mjumbe msaidizi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw.Wu Haitao ametoa wito wa msaada wa kimataifa kusukuma mbele maendeleo na upatikanaji wa amani Sudan Kusini.

    Ameeleza kuwa, utekelezaji wa makubaliano ya mwezi Septemba mwaka huu ya Makubaliano ya Amani na kuzindua upya maendeleo ya kiuchumi zinahitaji fedha na njia nyingine za misaada na kuongeza kuwa, jumuiya za kimataifa lazima zichukue hatua kutoa misaada ya kibinadamu na kiuchumi nchini humo.

    Wakati huo huo, mkuu wa Operesheni wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani Jean-Pierre Lacroix amesisitiza uanzishaji wa mpango wa usalama wa mpito baina ya serikali ya Sudan Kusini na upinzani ili kusukuma mbele mchakato wa amani baada ya makubaliano mapya ya amani mwezi Septemba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako