• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Watalii wanaofika Mombasa kwa ndege waongezeka

    (GMT+08:00) 2018-12-19 19:52:27

    Mashirika zaidi ya ndege ya kimataifa yameendelea kutua katika mji wa Mombasa nchini Kenya , yakileta watalii msimu kusherehekea msimu wa Krisimasi na mwaka mpya.

    Mkurungezi mkuu wa halmashauri ya utalii nchini Kenya Betty Radier amesema ongezeko la ndege za moja kwa moja kwenda kwenye uwanja wa kimataifa wa Moi ni ishara ya kutambulika kwa mji huo na watalii wan chi za magharibi, Marekani, na mashariki ya kati.

    Akipokea wageni 150 waliosafiria shirika la ndege la Qatar binbi Radier alisema KTB itashirikiana na shirika hilo ili kuongeza watalii mjini Mombasa na Kenya kwa jumla.

    Shirika la Ethiopia pia linafanya ziara za kila simu kati ya Mombasa a Addis Ababa.

    Mbali na mashirika ya ndege, Mombasa pia inapokea watalii wanaofika na meli zinazotia nanga kwenye eneo jipya la kuegeza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako