• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka: CAF kupanga Makundi ya michuano ya mataifa ya Afrika AFCON 2019 U-17

    (GMT+08:00) 2018-12-20 08:36:33

    Shirikisho la soka Afrika CAF leo katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam watapanga Makundi ya michuano ya mataifa ya Afrika AFCON 2019 kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 ambapo michuano hiyo inachezwa Tanzania wakiwa wenyeji. Jumla ya timu zitakazoshiriki fainali hizo za vijana wenye umri chini ya miaka 17 ni mwenyeji Tanzania, Angola, Cameroon, Guinea, Morocco, Nigeria, Senegal na Uganda na kama ilivyo kawaida timu nne zitakazofanikiwa kuingia nusu fainali zitafuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia U-17 nchini Peru mwaka 2019. Fainali hizo za mataifa ya Afrika zitakazochezwa Tanzania zitaanza April 14-28 2019 jijini Dar es Salaam. Michuano hiyo iliyofanyika Gabon mwaka 2017, Tanzania iliondolewa katika hatua ya Makundi, na leo ndio droo ya upangaji wa makundi mawili utachezeshwa Mlimani City Dar es Salaam wakiwa wajumbe wa CAF washakagua miundo mbinu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako