• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kazi ya kutokomeza tatizo la umaskini nchini China yaingia katika kipindi muhimu

    (GMT+08:00) 2018-12-20 16:46:53

    Mwaka 2018 ni mwanzo wa utekelezaji wa mipango ya China ya miaka mitatu kuhusu kuondoa kabisa umaskini, China imehimiza mambo ya kupunguza umaskini kwa nguvu isiyotarajiwa, na kupata mafanikio mazuri yanayofuatiliwa na dunia. Ikiwa imesalia miaka miwili kabla ya lengo la kuijenga China iwe na jamii yenye maisha bora kutimizwa mwaka 2020, China itachukua hatua gani muhimu katika kipindi kijacho?

    Tangu sera ya mageuzi na ufunguaji mlango ilipoanza kutekelezwa mwaka 1978, katika miaka 40 iliyopita, China imetekeleza mchakato muhimu wa kupunguza umaskini, na kuwawezesha watu zaidi ya milioni 700 vijijini kuondokana na umaskni, kiasi ambacho ni sawa na asilimia 10 ya idadi ya jumla ya watu duniani. Mwaka 2018 kiwango cha umaskini nchini China kinatarajiwa kupungua hadi chini ya asilimia 2, mafanikio hayo yamefuatiliwa na watu dunia nzima. Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Bw. Jim Yong Kim anaona uzoefu iliopata China katika hatua ya kupunguza umaskini unastahili kuigwa na dunia, anasema:

    "Katika miaka 40 iliyopita, China imepata mafanikio makubwa katika kupunguza umaskini ambayo hayakupatikana katika jamii ya binadamu. China inatazamiwa kutimiza lengo la kutokomeza kabisa umaskini ndani ya muda mfupi ujao. Kuna umuhimu mkubwa kwetu kukumbusha mafanikio hayo ya China. Kwani tunataka kujua jinsi China inavyopata mafanikio hayo, ambayo yataisaidia China kufanya vizuri zaidi mageuzi katika siku zijazo, wakati huo huo uzoefu wa China pia utazisaidia nchi nyingine kujiendeleza."

    Hivi saa kuna watu elfu 30 maskini vijijini wanaohitaji kuondokana na umaskini, wengi kati yao ni walemavu, wazee wasio na watu kuwatunza, wagonjwa, au watu wenye kiwango cha chini cha elimu, na wanaokosa uwezo wa kiufundi. Kwa mujibu wa Mpango wa mwaka 2018-2020 uliotolewa na serikali ya Chia kuhusu kupunguza umaskini, China itawasaidia watu hao kuondokana na umaskini kwa njia za kuendeleza uzalishaji, kuwahamishia kwenye makazi mapya, kutoa fidia, kuendeleza elimu na kutoa huduma za jamii. Mkurugenzi wa Ofisi ya upunguzaji umaskini ya Baraza la serikali la China Bw. Liu Yongfu anasema:

    "Hadi kufikia mwaka 2020, wastani wa pato kwa mtu maskini utazidi dola za kimarekani 580, ili kuondoa wasiwasi wa watu maskini kuhusu chakula, nguo, elimu ya lazima, huduma za kimsingi za matibabu na usalama wa makazi. Endapo masuala hayo hayatatatuliwa, itaonesha kuwa China haijaondokana kabisa na umaskini."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako