• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Algeria wapongezana kuhusu maadhimisho ya miaka 60 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kidiplomasia

    (GMT+08:00) 2018-12-20 16:53:52

    Rais Xi Jinping wa China na rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria leo wamepongezana kwa njia ya simu kuhusu maadhimisho ya miaka 60 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kidiplomasia.

    Rais Xi Jinping amezitaka China na Algeria kufanya maadhimisho ya miaka 60 kuwa mwanzo mpya, kuimarisha urafiki na ushirikiano, na kusukuma mbele uhusiano wa kiwenzi na kimkakati kati yao, ili kuzinufaisha nchi hizo mbili na wananchi wao.

    Rais Bouteflika amesema, Algeria inapenda kuimarisha uaminifu wa kisiasa kati yake na China, kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", kuunga mkono ujenzi wa Jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, na kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kufikia kiwango cha juu zaidi.

    Siku hiyo mawaziri wakuu wa China na Algeria pia wamepongezana kwa njia ya simu kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 60 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kidiplomasia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako