• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa afya wa China watoa mafunzo ya upasuaji kwa wenzao wa Uganda

    (GMT+08:00) 2018-12-20 18:21:17

    Wataalamu wa afya wa China wameanza kutoa mafunzo ya miezi mitatu ya upasuaji wa laparaskopiki kwa wahudumu 26 wa afya wa Uganda. Mafunzo hayo yanafanywa na timu ya madaktari bingwa kwa ushirikiano wa China na Uganda kupitia Shirika la ushirikiano wa kimataifa wa kiuchumi na kiufundi la Jiangxi la China.

    Mhandisi mkuu ambae pia ni mmoja wa wakufunzi toka China Ou Yuan ameeleza kuwa, mafunzo hayo yanalenga kuwafundisha wahudumu hao wa afya njia bora ya upasuaji wa laparoskopiki na kutumia vifaa vya kisasa ambavyo hutumia sehemu ndogo ya upasuaji wa mwili wa mgonjwa.

    Naye Bibi Regina Mugisa, mkuu wa hospitali hiyo amesema mafunzo hayo ya utaalamu na teknolojia mpya ya kisasa ya upasuaji yatawasaidia wahudumu hao wa afya kufanya kazi kwa ubora zaidi na kufanya upasuaji wa uhakika kwa wagonjwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako