• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wasafiri wa Fastjet kusaidiwa

  (GMT+08:00) 2018-12-20 19:52:24

  Baraza la Utetezi wa Wasafiri wa Anga (TCAACCC) limewahakikishia abiria wa Fastjet kuwa watapata haki zao. Taarifa hii inakuja siku moja tu baada ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kutangaza kusitisha kuruka kwa ndege za Fastjet.

  Katibu mtendaji wa baraza hilo, Deborah Mligo amesema wanachokifanya ni kuhakikisha kila anayestahili, anapata haki yake tena kwa wakati.

  Abiria walianza kurejeshewa nauli zao hapo jana huku wengine wenye tiketi wakitakiwa kufuata utaratibu kuhakikisha wanarudishiwa nauli zao.

  Baraza hilo limeingia kazini kuhakikisha kila abiria anapata haki yake wakati shirika hilo likiendelea kuweka mambo yake sawa ili iwapo litaweza, linusurike kupoteza leseni ya biashara.

  TCAA imeipa Fastjet notisi ya siku 28 kuthibitisha uwezo wake wa kujiendesha na kutoa huduma za uhakika kwa abiria.

  Baada ya kauli ya mamlaka hiyo, Fastjet ilitangaza kurudisha nauli za abiria na wadau wengine kuanzia Desemba 20.

  Kwa watakaopata usumbufu wowote, alisema wanaweza kuwasiliana na baraza hilo mara moja .

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako