• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapaswa kufungua mlango zaidi kutimiza maendeleo yenye ubora

    (GMT+08:00) 2018-12-21 09:50:35

    Kwenye mkutano wa maadhimisho ya miaka 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, rais Xi Jinping wa China alitoa majumuisho tisa ya uzoefu wa mageuzi na ufunguaji mlango, moja kati ya majumuisho hayo ni kuwa China inapaswa kufungua mlango zaidi na kuendelea kusukuma mbele ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, uzoefu ambao una umuhimu mkubwa katika kuuelekeza uchumi wa China kutimiza maendeleo yenye ubora.

    Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, rais Xi Jinping wa China amesisitiza mara nyingi kuwa China itaendelea kufungua mlango. Katika miezi kadhaa iliyopita, kiwango cha ushuru wa forodha cha China kimepungua hadi asilimia 7.5, na sekta nyingi zikiwemo fedha, magari, ndege na meli zimefunguliwa kwa mitaji ya nje, na kiwango cha ubora wa mazingira ya kibiashara ya China kimepanda kwa nafasi zaidi ya 30 ndani ya mwaka mmoja kwa mujibu ripoti ya Benki ya dunia.

    Rais Xi amesema kwenye hotuba yake kuwa ujenzi wa "Ukanda mmoja Njia moja" utakuwa jukwaa muhimu kwa China kutimiza maendeleo yenye ubora kwa upande wa ndani na nje, kwenye msingi wa kujadiliana kwa pamoja, kujenga kwa pamoja na kunufaika kwa pamoja. Katika miaka mitano iliyopita, thamani ya biashara kati ya China na nchi za "Ukanda mmoja, Njia moja" imezidi dola za kimarekani trilioni tano, uwekezaji wa moja kwa moja wa China kwa nje umezidi dola bilioni 60 na kutoa nafasi za ajira zaidi ya laki mbili, hali inayoonesha kuwa ujenzi wa "Ukanda mmoja, Njia moja" ni mkakati wa kunufaishana, si kama tu utakidhi mahitaji ya maendeleo ya nchi mbalimbali na unalingana na mpango wa China wa kuendeleza mageuzi na kufungua mlango, na bali pia umesukuma mbele ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako