• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka: Vijana wa Serengeti Boys U-17 waangukia mikononi mwa Nigeria, Uganda na Angola

    (GMT+08:00) 2018-12-21 09:55:25

    Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17 (U-17), imepangwa Kundi A pamoja na Nigeria, Uganda na Angola katika fainali za Mataifa Afrika kwa vijana U17 yatakayofanyika Aprili 14 hadi 28, 2019 nchini Tanzania. Droo ya upangaji wa makundi ya Mashindano hayo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa Mlimani City. Serengeti Boys itaanza kwa kucheza dhidi ya Nigeria kabla ya kuivaa Angola na kumaliza na majirani zake Uganda. Kundi B linaundwa na Guinea, Cameroon, Morocco na Senegal. Washindi wawili wa kila kundi watafuzu hatua ya nusu fainali ambayo pia inawawezesha kushiriki fainali za dunia mwakani nchini Peru.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako