• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka: Kocha wa Harambee Stars ya Kenya Sebastien Migne atishia kuikacha timu

    (GMT+08:00) 2018-12-21 09:55:44

    Kocha wa Harambee Stars Sebastien Migne huenda akaondoka Kenya na kuiacha Stars mashakani baada ya kudai hajapokea mishahara yake ya miezi kadhaa. Raia huyo wa Ufaransa amejikuta kwenye mazingira magumu sana ya kazi nchini Kenya licha ya serikali kusema kuwa imemlipa lakini hajapata pesa katika akaunti zake. Shirikisho la Soka Kenya kupitia kwa afisa wake wa habari Barry Otieno, Jumanne, Disemba 18, alithibitisha kuwa, Migne hajalipwa tangu Oktoba. Lakini mwanzoni mwa wiki hii, serikali ilisema imemlipa Migne mishahara yake ya Septemba na Oktoba ambazo ni kiasi cha KSh 3 Milioni. Migne atakuwa kocha wa kwanza kuondoka baada ya Stars kufuzu michuano ya AFCON na kusaidia viwango vya soka kuimarika. Wakati huohuo Harambee Stars imesalia katika nafasi ya 105 iliyoshikilia mwezi Novemba mwaka 2018 kulingana na orodha iliyotolewa na Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA jana kwa kujizolea alama 1210, hii ikiwa ni alama sawa na iliyopata mwezi Novemba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako