• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Riadha: StarTimes yamtunukia zawadi nono mkimbiaji Mary Keitany

    (GMT+08:00) 2018-12-21 09:58:31

    Bingwa mara nne wa Marathon ya New York City Mary Keitany juzi alitajwa na StarTimes Sports kama mchezaji bora wa mwezi November.

    Keitany mwenye miaka 36 alijishindia taji lake la nne kwenye Marathon ya New York City mwezi November akitumia muda wa 2:22:48, akivunja rikodi ya marathon ya New York. Keitany amechukua ushindi mwaka 2014, 2015, 2016 na 2018. Siku ya Jumanne Keitany pia alitajwa mkimbiaji bora wa New York wa mwaka 2018, baada ya kupata ushindi wake wa nne kwenye Marathon ya New York. Keitany amemshinda dereva wa langalanga Carl "Flash" Tundo, aliyejipatia ushindi wake wa sita kwa msimu huu. Wengine waliokuwepo kwenye kinyangányiro hicho cha mwezi Novemba ni Samuel Njoroge, aliyeshinda Michuano ya wazi ya tenisi ya Lagos na Wanamashumbwi wa Kenya wakiwemo Black-Moses Mathenge, Nick Okoth, Isaac Meja, Simon Mulinge, na Fredrick Onyango ambao wote walishinda medali za fedha katika michezo ya wanajeshi ya Afrika nchini Morocco. Keitany ameondoka na kombe, televisheni ya dijitali ya inchi 43 ya StarTimes na fedha taslimu Sh100, 000 za Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako