• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga Marekani kupitisha sheria kuhusu Tibet

    (GMT+08:00) 2018-12-21 10:12:19

    China imepinga vikali uamuzi wa Marekani kupitisha sheria kuhusu masuala ya ruhusa kwa wageni kuingia Tibet. Bunge la umma la China jana usiku lilitoa taarifa ikieleza kukasirishwa na kupinga vikali kitendo hicho cha Marekani, na kusema kinachafua sera ya kufungua mlango ya China kuhusu mambo ya Tibet, na kuweka sera ya visa yenye ubaguzi dhidi ya maofisa wa China, na pia inakiuka kanuni ya kimsingi ya uhusiano wa kimataifa kwa kuingilia mambo ya ndani ya China. Aidha, taarifa hiyo inasema kitendo hicho cha Marekani kimetoa ishara yenye makosa makubwa kwa wafarakanishaji wa Tibet.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China bibi Hua Chunying amesema, mambo ya Tibet ni mambo ya ndani ya China, China hairuhusu nchi yoyote kuingilia mambo hayo, na kitendo hicho cha Marekani kitaleta athari hasi kwa mawasiliano na ushirikiano kati yake na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako