• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China atoa maoni kuhusu kauli na vitendo vyenye makosa vya Marekani kuhusu suala la usalama la tovuti ya internet

    (GMT+08:00) 2018-12-21 18:32:52

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo ametoa maoni kuhusu kauli na vitendo vyenye makosa vya Marekani kuhusu suala la usalama la tovuti ya internet.

    Bibi Hua amesema kuwa Marekani ilitunga uwongo na kuilaani China katika suala la usalama la tovuti ya internet bila ya msingi, na kuwashtaki wachina wawili kwa makosa ya kuiba siri kwenye tovuti ya internet, hatua ambayo imekiuka vibaya utaratibu wa kimsingi wa uhusiano wa kimataifa na kuathiri vibaya ushirikiano kati ya China na Marekani, China inakipinga kithabiti.

    Bibi Hua alisema kuwa serikali ya China haijihusishi au kuunga mkono mtu yeyote kuiba siri ya biashara. China inaihimiza Marekani kusahihisha makosa yake na kusimamisha kuikashifu China kwenye suala la usalama la tovuti ya interet, na kuondoa mashtaka kwa wachina hao. China itachukua hatua za lazima ili kulinda usalama wa tovuti ya internet na maslahi yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako