• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito wa msaada wa kimataifa kusaidia nchi za Sahel

    (GMT+08:00) 2018-12-21 19:03:17

    Mjumbe msaidizi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia nchi za ukanda wa Sahel zilizo kaskazini mwa Afrika upatikanaji wa amani na maendeleo ya kiuchumi.

    Ameeleza kuwa, ugaidi, uhalifu wa kimataifa unaopangwa, umaskini, kutokuwa na usawa wa kikanda pamoja ya matatizo yanakwamisha amani na maendeleo katika sehemu hiyo.

    Bw. Wu amesema hali ilivyo sasa inahitaji nguvu zaidi na mbinu kamili za jumuiya ya kimataifa, na kuomba juhudi za kimataifa kutafuta muafaka wa kisiasa kwa masuala makubwa ya kikanda ili kupata utulivu, mazingira ya amani na maendeleo ya muda mrefu.

    Pia amesisitiza kuwa China itaendelea kusaidia nchi za Sahel kutimiza amani na ustawi wa kudumu.

    Mkutano wa Baraza la Usalama ulihusisha nchi tano zikiwemo Burkina Faso, Chad, Mali, Mauritania na Niger, ambazo zimeanzisha nguvu ya pamoja ya kijeshi ili kupambana na ugaidi katika kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako