• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sehemu ya Pili ya Makala za vielelezo za Lugha ya Kichina zilizosomwa imewekwa kwenye mtandao

    (GMT+08:00) 2018-12-23 18:12:13

    Tarehe 23 Desemba, mkutano wa kutangaza Sehemu ya pili ya Makala za vielelezo za Lugha ya taifa la China zilizosomwa ambazo zinatumika kwenye shule za sekondari na shule za msingi umefanyika hapa Beijing. Mkutano huo umeandaliwa na Kituo kikuu cha Radio na Televisheni cha taifa pamoja na Wizara ya elimu na Kamati ya lugha ya taifa. Naibu mkuu wa Idara ya uenezi ya Kamati kuu ya Chama ambaye pia ni Mkuu wa Kituo kikuu cha Radio na Televisheni cha taifa Bw. Shen Haixiong, na naibu waziri wa elimu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kamati ya lugha ya taifa Bw. Du Zhanyuan wamehudhuria mkutano huo, na kushuhudia Sehemu ya Pili ya makala 100 za vielelezo za lugha ya taifa la China zilizosomwa zikiwekwa kwenye mtandao.

    Maktaba kwenye mtandao ya makala za vielelezo za lugha za taifa la China inatoa makala za mafunzo zilizosomwa kwa Kichina sanifu kwa shule za sekondari na shule za msingi kote nchini, makala hizo zilisomwa na watangazaji hodari wapatao zaidi ya 100 wa Kituo kikuu cha Radio na Televisheni cha taifa, na kunaswa sauti na kutengenezwa kuwa video na mafundi wenye ustadi wa hali ya juu. Makala hizo ni zawadi za mwaka mpya kwa wanafunzi wa shule za sekondari na shule za msingi za nchi nzima. Aidha, Kituo kikuu cha Raido na Televishen cha taifa na Wizara ya elimu ya China pia zimezawadia sehemu za vijijini na milimani vyombo vya kutazama video hizo.  

    "Maktaba ya makala za vielelezo za lugha ya taifa la China zilizosomwa ambazo zinatumiwa kwenye shule za sekondari na shule za msingi", si kama tu ina umuhimu wa kutoa vielelezo vya matamshi ya lugha ya Kichina sanifu, zaidi ni kueleza mtazamo sahihi kuhusu maadili, na kuenzi utamaduni mzuri wa jadi wa China, ili wanafunzi wa shule za sekondari na shule za msingi waongeze imani juu ya utamaduni na kuongeza nguvu ya utamaduni wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako