• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yatakiwa kutoa maelezo kuhusu balozi zake kununua vifaa vya kijasusi

    (GMT+08:00) 2018-12-25 09:30:05

    Nyaraka zilizotolewa hivi karibuni na tovuti ya Wikileaks zimeonesha kuwa, balozi za Marekani katika nchi nyingi zimewahi kununua vifaa vya kijasusi. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying jana alisema Marekani haijatoa maelezo kuhusu tukio la mpango wa PRISM lililotokea miaka 5 iliyopita, hivi sasa tovuti ya Wikileaks imefichua nyaraka mpya, na Marekani pia inatakiwa kutoa maelezo kuhusu tukio hilo kwa jumuiya ya kimataifa.

    Bibi Hua amesema Marekani inatakiwa kutoa maelezo kuhusu sababu za balozi zake kununua vifaa hivyo, vitatumika kwa malengo gani na kuwalenga watu gani. Amesema Marekani pamoja na washiriki wake karibuni zilishutumu China kuhujumu usalama wa mtandao wa Marekani, na nyaraka zilizotangazwa na tovuti ya Wikileaks zimeonesha kuwa, Marekani ndiyo inayoharibu usalama wa mtandao wa internet wa nchi nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako