• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kuchangia zaidi bajeti ya Umoja wa Mataifa

  (GMT+08:00) 2018-12-25 17:02:32

  Baraza kuu la Umoja wa Mataifa hivi karibuni lilipitisha azimio la kuongeza mchango wa China kwa bajeti ya kawaida ya umoja huokutoka asilimia 7.9 na kuwa asilimia 12.01, na bajeti ya kulinda amani ya umoja huo kutoka asilimia 10.2 kuwa asilimia 15.2, na China itakuwa mchangiaji mkubwa wa pili kwa bajeti ya Umoja wa Mataifa.

  Huu ni mwaka wa 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, na wastani wa asilimia 9.5 kwa mwaka wa ongezeko la uchumi umeifanya China ibadilike kuwa moja ya nchi yenye nguvu zaidi kutoka nchi maskini. Katika miaka 10 iliyopita, China imetuma vikosi 31 vya manowari kutoa ulinzi katika bahari ya Somalia na ghuba ya Aden, na kushiriki kwenye operesheni 30 za kulinda amani za Umoja wa Mataifa.

  Mwaka 2013, rais Xi Jinping wa China alitoa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", ambalo ni wazo jipya la kuhimiza maendeleo ya dunia. Ingawa baadhi ya nchi za magharibi zinapaka matope pendekezo hilo, lakini katika miaka mitano iliyopita, zaidi ya nchi 100 zimejiunga na pendekezo hilo, na nchi na mashirika ya kimataifa zaidi ya 70 wamesaini makubaliano ya kibiashara na China kuhusu pendekezo hilo.

  Takwimu zilizotolewa na Kamati ya Uwekezaji ya Ethiopia zinaonesha kuwa, kuanzia mwaka 2012 hadi 2017, kampuni 279 za China zimeanzisha shughuli nchini Ethiopia, na kuleta ajira 28,300 kwa nchi hiyo. Gazeti la Daily Nation la Kenya lilitoa tahariri ikisema China ni mwenzi mwenye thamani kwa Afrika, na inajitahidi kuondoa umaskini uliodumu kwa karne kadhaa barani Afrika. Jumuiya maarufu ya washauri bingwa ya Marekani Brookings Institute, inaona kuwa uwekezaji wa China unaweza kusafisha njia kwa ajili ya maendeleo shirikishi duniani, na miradi ya msaada ya China katika nchi zinazoendelea imeleta manufaa makubwa.

  Mwaka huu, ongezeko la vitendo vya upande mmoja, kujilinda kibiashara, na kupinga utandawazi limeleta changamoto kubwa kwa utaratibu wa kimataifa na mfumo wa kibiashara duniani. Wakati huohuo mivutano ya kibiashara iliyochochewa na Marekani imesababisha hali ya msukosuko kwenye soko la mitaji, na athari mbaya kwa uchumi wa dunia.

  Hivi sasa uchumi wa dunia na mageuzi ya mfumo wa kushughulikia masuala ya kimataifa viko katika njia panda, na jumuiya ya kimataifa yenye wasiwasi kuhusu mustakbali wa baadaye inahitaji uongozi bora. Uongozi huo unatokana na uhusiano mpya wa kimataifa wenye haki, usawa, ushirikiano na kanuni ya kuheshimiana.

  Wakati China itakapokuwa mchangiaji mkubwa wa pili wa bajeti ya Umoja wa Mataifa, dunia inaweza kutambua kuwa, kwa kushirikiana na nchi nyingine, inapenda kutoa mchango zaidi kwa ajili ya kujenga dunia mpya yenye amani ya kudumu, usalama, ustawi wa pamoja, masikilizano na mazingira mazuri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako