• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yapongezwa kwa kulinda usalama wa ghuba ya Aden

  (GMT+08:00) 2018-12-26 17:20:57

  Katika miaka 10 iliyopita, manowari za China zimetoa ulinzi kwa ajili ya meli za nchi mbalimbali zilizopita ghuba ya Aden, na kusifiwa na jumuiya ya kimataifa. Ghuba ya Aden ni njia pekee ya kuunganisha bahari ya Hindi na Bahari Nyekundu, na inapitiwa na meli zaidi ya elfu kumi kwa mwaka. Kutokana na mashambulizi ya maharamia, ghuba hiyo ni moja kati ya sehemu yenye hatari zaidi duniani.

  Kwa kufuata azimio la Umoja wa Mataifa, katika miaka 10 iliyopita, jeshi la baharini la China limetuma manowari 100 katika vikundi 31, helikopta 67, na zaidi ya askari 26,000 kutoa ulinzi katika ghuba hiyo.

  Mwezi Aprili mwaka 2017, ghuba hiyo iliyokuwa na utulivu kwa muda mrefu ilifuatiliwa tena, meli ya mizigo ya OS35 ya iliyosajiliwa nchini Tuvalu ilitekwa nyara na maharamia. Manowari ya Yulin ya China ilipelekwa, na kufanikiwa kuiokoa meli hiyo. Baharia mmoja aliyeokolewa anasema,

  "Kulikuwa na manowari tano, lakini manowari ya China pekee ndio ilikuja kutuokoa. Naishukuru China, na washukuru askari wa China."

  Katika miaka 10 iliyopita, manowari za China zimetoa ulinzi kwa ajili ya meli zaidi ya 6,600, kuziokoa zaidi ya meli 70, kufukuza mashua zaidi ya 3,000 za maharamia, na kuwakamata maharamia watatu. Licha ya kutoa ulinzi, manowari za China pia zinatoa misaada mingine. Mwezi Disemba mwaka 2014, mji wa Male wa Maldives ulikumbwa na upungufu wa maji baridi, manowari ya Changxingdao ya China iliyokuwa ikitoa ulinzi baharini ilipeleka maji zaidi ya tani 600 kwa mji huo. Kapteni wa manowari hiyo Bw. Hu Jinkai anasema,

  "Tulipata maji hayo kwa kubana matumizi yetu. Lakini naona hili ni jambo la kawaida, sisi ni marafiki, tunasaidiana."

  Katika miaka hiyo 10, manowari za China zilitoa ulinzi kwa ajili ya meli 3,400 za nchi za nje, ambazo zinachukua asilimia 51.5 ya meli zote zilizolindwa. Manowari za China pia zimeanzisha ushirikiano mzuri na manowari za nchi nyingine.

  Mtaalamu wa mambo ya kijeshi Bw. Zhang Junshe anaona kuwa, manowari za China zimetoa mchango muhimu kwa ajili ya kulinda amani na utulivu duniani kwa kutoa ulinzi katika ghuba ya Aden ambayo ni njia muhimu ya kibiashara baharini. Anasema,

  "Kazi ya kulinda usalama ya manowari za China katika miaka 10 iliyopita imethibitisha kuwa China ni nchi kubwa inayowajibika, na maendeleo ya majeshi ya China yatanufaisha amani na usalama duniani."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako