• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuharakisha utekelezaji wa hatua za kufungua mlango zaidi kwa sekta ya uzalishaji

    (GMT+08:00) 2018-12-26 19:19:04

    Naibu waziri wa viwanda na teknolojia ya habari wa China Bw. Xin Guobin hivi karibuni amesema, sekta ya uzalishaji ni jambo muhimu la uchumi halisi, katika siku za usoni China itahimiza mageuzi bora, ufanisi na motisha ya sekta ya uzalishaji, na kuharakisha utekelezaji wa hatua za kufungua mlango zaidi kwa sekta hiyo.

    Bw. Xin aliyasema hayo kwenye mkutano wa mwaka 2018 kuhusu uchumi wa China uliofanyika hivi karibuni. Amesema kwa sasa sekta ya uzalishaji ya China ni kubwa lakini haina nguvu kubwa, hali ya jumla ya kutokuwa na teknolojia na vifaa muhimu haijabadilika, na hali ya kuwa katika ngazi ya chini ya mnyororo wa thamani duniani haijabadilika.

    Mkutano wa kazi ya uchumi wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China umetoa kipaumbele katika kuhimiza maendeleo yenye sifa bora ya sekta ya uzalishaji mwaka 2019, na kutoa hatua mbalimbali za kuhimiza maendeleo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako