• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wang Yi kufanya ziara nchini Ethiopia, Burkina Faso, Gambia na Senegal na makao makuu ya Umoja wa Afrika

    (GMT+08:00) 2018-12-28 19:14:02

    Msemaji wa waziri wa mambo ya nje wa China bibi Hua Chunying amesema kuwa, mjumbe wa taifa ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi atafanya ziara nchini Ethiopia, Burkina Faso, Gambia na Senegal pamoja na Makao makuu ya Umoja wa Afrika.

    Bw. Wang Yi atafanya ziara hizo kuanzia tarehe 2 hadi 6 Januari mwakani, na atakutana na baadhi ya viongozi wa nchi hizo na Umoja wa Afrika.

    Bibi Hua amesema hii itakuwa mara ya kwanza kwa waziri wa mambo ya nje wa China kufanya ziara barani Afrika baada ya mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, na madhumuni ya ziara hizo ni kuhimiza utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako