• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chombo cha uchunguzi cha Changé-4 cha China kimebadili mzunguko wa obiti na kujiandaa kutua

    (GMT+08:00) 2018-12-30 16:21:13

    Idara ya Taifa ya Anga ya Juu ya China CNSA imetangaza kuwa chombo cha uchunguzi cha Changé-4 cha China leo asubuhi kimeingia kwenye obiti kama ilivyopangwa ili kujiandaa kutua katika upande wa mwezi usioonekana duniani.

    Tangu chombo cha Changé-4 kiingie kwenye mzunguko wa mwezi Disemba 12, kituo cha kuongozea duniani cha Beijing kimesawazisha chombo hicho mara mbili na kukifanyia majaribio kiungo cha mawasiliano kati ya chombo hicho na satelite ya Queqiao au Daraja la Magpie, inayosafirisha mawasiliano. Kulingana na CNSA kituo cha kuongozea kitachagua muda muafaka wa kukifanya chombo hicho kitue mwezini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako