• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka: Taifa Stars yaomba kuifunga Uganda Machi 3 ili iifuzu fainali za Afcon

    (GMT+08:00) 2018-12-31 08:55:56

    Kuna kila dalili kwamba Taifa Stars ikimfunga Uganda Machi 3 mwakani, itafuzu kwenye fainali za Afcon ambazo zina nafasi kubwa ya kufanyika Misri badala ya Morocco na Afrika Kusini. Stars inahitaji ushindi kwenye mchezo huo huku ikiombea Cape Verde itoke sare na Lesotho nyumbani au kushinda mechi hiyo. Habari za uhakika zinaeleza kuwa, Januari 9 Misri ina nafasi kubwa ya kutangazwa kuwa mwenyeji wa Afcon baada ya Cameroon kupigwa chini. Ingawa Afrika Kusini nao wanawania nafasi ya kuandaa fainali hizo sawa na Morocco lakini Misri inapewa nafasi kubwa mpaka sasa kwakile kilichoelezwa kwamba miundombinu yao ipo tayari. Mmoja wa vigogo wa CAF Amaju Pinnick alisema watazingatia kigezo cha nchi iliyo tayari kimiundombinu kwavile muda uliobaki ni mdogo

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako