• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka: Caf yaipeleka Nkana FC ya Zambia mdomoni mwa Waivory Coast

  (GMT+08:00) 2018-12-31 08:56:29

  Shirikisho la Soka Afrika (Caf), limempeleka beki wa kimataifa wa Tanzania, Hassan Kessy na timu yake ya Nkana FC ya Zambia mdomoni mwa Waivory Coast baada ya timu hiyo kuangukia kucheza mechi ya mchujo ili kusaka nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Nkana iliyotolewa na Simba katika raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ni miongoni mwa timu zilizoangukia kucheza mechi hizo za mchujo ambazo droo yake ilifanyika juzi na kupangwa kucheza dhidi ya FC San Pedro ya Ivory Coast. Na kwa upande wa wawakilishi wa Afrika Mashariki kwenye michuano ya Kombe la Shririkisho Afrika, Gor Mahia ya Kenya, Vipers SC na KCCA za Uganda zimepangiwa wapinzani wagumu katika mechi za mchujo kuwania kucheza hatua ya makundi ya kinyang'anyiro hicho. Timu 15 zitakazopata ushindi wa jumla wa mechi ya nyumbani na ugenini, zitaungana na Etoile du Sahel ya Tunisia katika hatua ya makundi ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Janauri mwakani

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako