• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tuzo: Peter Munuve na Jane Ndenga wateuliwa tena kwenye tuzo za mwanamichezo bora wa mwaka

  (GMT+08:00) 2018-12-31 08:56:46

  Nyota wa tenisi Peter Munuve na Jane Ndenga ambao ni walemavu wameteuliwa kwa mara nyingine tena kwenye tuzo za mwanamichezo bora wa mwaka. Hata hivyo Munuve, ambaye aliteuliwa kwa mara ya kwanza kwenye tuzo za mwaka 2017, atalazimika kumshinda mchezaji wa mpira wa mikono Dickson Ondwari kwa upande wa tuo za wanaume. Pia katika kitengo hicho kuna mkimbiaji wa kiti cha magurudumu Samuel Kuria na Henry Caleb Otieno. Mshindi atajulikana kwenye sherehe zilizopangwa kufanyika Januari 11, 2019 huko Mombasa. Kwa upande wa tuzo za wanawake, Ndenga, ambaye amewahi kuteuliwa mara tatu, anakabiliana na mlinda mlango wa timu maalumu ya sokaya Olimpiki ya Kenya Michelle Kaindi na wakimbiaji wa kiti cha magurudumu Caroline Wanjira, Eunice Adhiambo na Asia Mohammed.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako