• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Marekani zafanya juhudi kupunguza tofauti na kupanua maoni ya pamoja kupitia ushirikiano

    (GMT+08:00) 2018-12-31 09:19:14

    Rais Xi Jinping wa China tarehe 29 alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na rais Donald Trump wa Marekani, na kupeana salama za mwaka mpya, na kutaka pande hizo mbili zifikie makubaliano ya kunufaishana na kuinufaisha dunia.

    Habari zinasema katika mwezi huu pande hizo mbili zimefanya juhudi kuhimiza maafikiano yaliyofikiwa na marais hao wawili walipokutana nchini Argentina. Licha ya kufanya majadiliano ya ngazi ya naibu mawaziri kuhusu uwiano wa biashara na ulinzi wa haki miliki, China pia ilianza tena kununua mazao ya kilimo ya Marekani na kutangaza kusimamisha kuongeza ushuru kwa magari na vipuri vya magari vya Marekani. Hivi sasa pande hizo mbili zinapanga kuanzisha tena mazungumzo ya ana kwa ana na kuhimiza kutekeleza makubaliano ya marais hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako