• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kituo kikuu cha radio na televisheni cha China chachagua habari kumi muhimu za ndani mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2018-12-31 17:07:37

    Kituo kikuu cha radio na televisheni cha China kimechagua habari kumi muhimu za ndani kwa mwaka 2018, ambazo ni zifuatazo:

    1. Muswada wa Marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Watu wa China walipitishwa, na fikra ya rais Xi Jinping wa China kuhusu ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya yaliandikwa kwenye katiba.

    2. Viongozi wa awamu mpya wa serikali na Baraza la mashauriano ya kisiasa la China walichaguliwa kuanzia tarehe 14 hadi 10 Mwezi Machi, na rais wa China Xin Jinping alikula kiapo kikatiba baada ya kuchaguliwa kwa muhula mwingine, na kuwa rais wa kwanza wa China kufanya hivyo katika historia.

    3. China ilisherehekea Maadhimisho ya miaka 40 tangu ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango tarehe 18 Mwezi Disemba.

    4. Mpango wa kuimarisha mageuzi kwa taasisi za Chama na serikali ya China ulitangazwa tarehe 21 Machi, hatua ambayo imeonesha kuwa mageuzi ya China yameingia kwenye kipindi kipya.

    5. Serikali kuu ya China ilichukua hatua mbalimbali kuhimiza maendeleo ya uchumi wa sekta binafsi. Rais Xi Jinping wa China alipohutubia Kongamano la mashirika binafsi lililofanyika tarehe 1 Novemba mjini Beijing, alisisitiza kuwa hadhi ya sekta binafsi kwenye maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya China haijabadilika, mkakati wa China wa kuunga mkono maendeleo ya sekta binafsi haujabadilika, na sera ya China ya kuboresha mazingira na kuongeza fursa kwa ajili ya sekta binafsi hazijabadilika.

    6. Shughuli mbalimbali za kidiplomasia zilizofanywa na China zaonesha hadhi ya China kuwa nchi kubwa duniani. Rais Xi Jinping wa China amefafanua wazo la kujenga Jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja katika mikutano mikubwa minne iliyofanyika China mwaka huu, yaani Mkutano wa mwaka 2018 wa Asia wa Bo'ao, Mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO, Mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, na Maonesho ya kwanza ya uagizaji bidhaa ya kimataifa ya China.

    7. Gwaride la ukaguzi wa jeshi la majini la China lilifanyika Aprili 12 kwenye bahari ya kusini ya China, ambalo ni gwaride kubwa zaidi la jeshi la China kufanyika baharini katika historia.

    8. Uhifadhi wa mazingira ya asili wapewa kipaumbele katika mchakato wa kuendeleza Ukanda wa kiuchumi wa Mto Changjiang.

    9. Muswada wa Marekebisho ya sheria ya kodi ya mapato ulipitishwa tarehe 31 Agosti kwenye kikao cha tano cha kamati ya kudumu ya Bunge la umma la China, huku hatua mbalimbali za kuboresha maisha ya watu zikitekelezwa.

    10. China ilianza kutunga sheria ya usimamizi wa chanjo, baada ya kashfa ya kampuni moja ya chanjo kutoa chanjo zisizofikia vigezo, kufichuliwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako