• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa China na Urusi watumiana salamu za Mwaka Mpya

    (GMT+08:00) 2018-12-31 17:09:03
    Rais Xi Jinping na mwenzake Vladmir Putin,Jumatatu hii wametumiana salamu maalum za kuukaribisha mwaka mpya wa 2019.

    Katika ujumbe wa pongezi kwa Rais Putin, Rais Xi amesema mwaka 2018 ulikuwa wenye mafanikio makubwa katika uhusiano kati China na Russia, kila moja kati ya nchi hizo mbili, imetekeleza kwa ufasaha mipango muhimu ya kisiasa ya kitaifa, na kufungua zama mpya za uhusiano kati ya China na Russia.

    Kwa upande wake Rais Putin, yeye ametuma salamu za kumtakia heri ya mwaka mpya Rais Xi, na kuwatakia furaha na afya njema raia wa China.

    Mwaka 2019, China na Russia zitaadhimisha miaka 70 tangu zianzishe uhusiano wa kidiplomasia, Rais Putin amesema anaamini kuwa hiyo itakuwa fursa ya kuendeleza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili na kuendelea kushughulikia masuala ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako