• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Maaabra kufungiwa kwa kutolipa kodi Tanzania

  (GMT+08:00) 2018-12-31 18:42:47

  Serikali ya Tanzania imetangaza kuzifungia maabara 719 zilizopo katika vituo vya afya binafsi ifikapo Januari 15, 2019 na wamiliki wake watashtakiwa.

  Uamuzi huo umetolewa kutokana na maabara hizo kutojiandikisha katika bodi ya usimamizi wa maabara binafsi za afya (PHLB) pamoja na kuwa na malimbikizo ya ada na tozo.

  Mkurugenzi wa tiba ya Wizara ya Afya, Dk Dorothy Gwajima amesema hadi Septemba 2018, PHLB ilikuwa inazitambua maabara 641 zinazojitegemea na 719 zilizopo kwenye vituo vya tiba vya watu binafsi.

  Dk Gwajima amesema bodi imebaini baadhi ya wamiliki wa maabara binafsi hususan zilizopo katika vituo vya tiba kutofuata maadili ya uwajibikaji kisheria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako