• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Mwanamitindo kutangaza utalii wa Tanzania

  (GMT+08:00) 2018-12-31 18:45:53

  Mwanamitindo na mwigizaji maarufu wa Marekani, Marisela De Montecristo, atazuru Tanzania mapema mwaka 2019 kusaidia kutangaza utalii nchini humo.

  Marisela ambaye ni raia wa El Salvador aliyehamia Los Angels, Marekani, atawasili Tanzania Januari 15 mwaka 2019, na kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, na ile ya Ngorongoro.

  Baada ya safari ya siku mbili katika hifadhi hizo atarejea Moshi Januari 22 na kutembelea moja ya kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kuona namna ya kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.

  Mwaka huu, Merisela ameshiriki mashindano ya ulimbwende nchini El Salvador na kufanikiwa kutwaa taji la Miss El Salvador 2018.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako