• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka: Yanga kutopeleka kikosi chake cha kwanza kombe la Mapinduzi

  (GMT+08:00) 2019-01-01 09:08:48

  Kuelekea michuano ya kombe la Mapinduzi inayoanza leo Januari 1, 2019 visiwani Zanzibar, klabu ya Yanga haitapeleka kikosi chake cha kwanza kwenye mashindano hayo. Kwa mujibu wa habari baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza wamepewa mapumziko na kocha Mwinyi Zahera ili kujiweka sawa kwa ajili ya mechi za ligi kuu. Miongoni mwa wachezaji ambao hawatakwenda ni kinara wa mabao wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu, Heritier Makambo, pamoja na Ibrahim Ajib na wachezaji wengine. Katika michuano hiyo ambayo inatarajiwa kufikia tamati Januari 13, Yanga imepangwa kwenye Kundi B na timu za KVZ, Malindi, Jamhuri, Azam na Yanga.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako