• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka: Rais wa Shirikisho la Soka la Afghanistan akanusha tuhuma za kuwanyanyasa kingono na kuwapiga wachezaji wanawake

  (GMT+08:00) 2019-01-01 09:09:05

  Rais wa Shirikisho la Soka la Afghanistan Keramuddin Karim jana alikanusha madai ya kuwanyanyasa kingono na kuwapiga wachezaji wa timu ya soka ya taifa ya wanawake, akisema watu wanaomshutumu wametoa madai hayo ili yaweze kuwasaidia maombi yao ya kutafuta hifadhi Ulaya. Katika madai yaliyoripotiwa kwa mara ya kwanza na gazeti la Guardian la Uingereza mwezi Novemba, Karim ambaye amesimamishwa kazi kama rais wa Shirikisho la Soka la Afghanistan (AFF) akisubiri matokeo ya uchunguzi amekuwa akishutumiwa kwa kuwapiga ngumi, kuwabaka na kuwatishia wachezaji wa kike, ikiwemo kuwalenga bastola kichwani. Kwa sasa uchunguzi bado unaendelea, lakini kwenye mahojiano aliyofanya na AFP alikuwa na uhakika kuwa jina lake litasafishwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako