• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tenisi: Federer aonesha hamu kubwa ya kupambana na Serena Williams Kombe la Hopman

  (GMT+08:00) 2019-01-01 09:11:18

  Mshawasha mkubwa umeibuka kwenye Kombe la Hopman baada ya wachezaji nguli wa mchezo wa tenis kukutana kwenye mechi ya wanawake na wanaume (Mpambano wa Jinsia) tangu uanzishwe miaka ya 1970. Roger Federer na Serena Williams, wachezaji tajika katika historia, watapambana kwa mara ya kwanza leo wakati Marekani itakapovaana na bingwa mtetezi Uswizi. Federer amesema ana uzoefu mkubwa wa kucheza dhidi ya wanawake. Hata hivyo amesema mbali na shughuli zao za michezo na kuhudhuria tafrija chache za mabingwa huko Wimbledon hamjui vizuri Serena. Naye Williams kupitia mahojiano kwenye televisheni amesema ana hamu kubwa sana ya kupiga picha na Federer ili aweke kwenye ukurasa wake wa Instagram.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako