• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sehemu mbalimbali nchini China zasherehekea kwa furaha Sikukuu ya Mwaka Mpya

    (GMT+08:00) 2019-01-01 17:09:22

    Tumeuaga mwaka 2018 wenye mafanikio huku tukikaribisha mwaka 2019 wenye matumaini makubwa. Wakati wa kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya, wachina wana furaha tele na pia matumaini na imani kubwa.

    Mjini Beijing, kwenye Bustani ya Olimpiki watu zaidi ya elfu tano kutoka hali mbalimbali wamjumuika pamoja kukaribisha kuwadia kwa mwaka mpya.

    Wakati kengele ya mwaka mpya ikilia, watu kutoka sehemu mbalimbali nchini na duniani walipeana heri ya mwaka mpya kwa kukumbatiana.

    Mjini Lanzhou, mkoa wa Gansu, watalii wengi wamemiminika kwenye njia ya Zhangye. Mwuzaji mmoja kwenye njia hiyo Wang Guangzhen anasema:

    "Mtoto wangu wa kiume amefaulumtihani wa kuingia chuo kikuu, nina furaha isiyoweza kusimulika. Natumai atasoma vizuri. Kama unataka kuishi maisha mazuri unapaswa kujitahidi, kwani hakuna chapati inayoweza kuanguka kutoka mbinguni."

    Kununua maua ni desturi ya wakazi wa mkoa wa Fujian. Soko la maua lenye historia ya zaidi ya miaka 1000 lililoko kwenye mtaa wa Qixiang mjini Fuzhou, limewavutia wakazi na watalii maelfu kadhaa. Bw. Huang Jianmin ni mkazi wa mji wa Fuzhou, matumaini yake ya mwaka mpya ni kuwa, chini ya uongozi wa chama cha kikomunisti cha China, mageuzi ya China yataweza kuimarishwa, na kuhimiza nchi iwe na uwezo mkubwa zaidi.

    Katika mji wa Kunming, mkoani Yunnan, maua ya aina mbalimbali yamepambwa kote mjini. Mtalii Huang Zhiling anasema:

    "Tangu nchi yetu ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango,imepata mafanikio na mabadiliko makubwa katika miaka 40 iliyopita . Nimerudi kutoka nchi za nje, lakini naona nchi yetu ni nzuri zaidi."

    Wakati huo huo wakazi wa vijijini pia wanafanya shughuli mbalimbali kama vile kucheza ngoma ya jadi na kuimba opera za kienyeji ili kusherehekea maisha yao mazuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako