• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Shen Haixiong atoa salamu za mwaka mpya kwa wasikilizaji

    (GMT+08:00) 2019-01-01 17:46:33

    Tarehe 1 Januari mwaka 2019, Mkuu wa Kituo kikuu cha Radio na Televisheni cha taifa cha China Bw. Shen Haixiong ametoa salamu za mwaka mpya kwa wasikilizaji wetu walioko sehemu mbalimbali kote duniani kwa kupitia matangazo kwenye radio, televisheni na mtandao wa internet. Bw. Shen amesema, kutoa habari za China kwa dunia, kutangaza habari za dunia kwa China, na kuongeza maelewano na urafiki kati ya wananchi wa nchi mbalimbali, hayo yote siku zote ni nia ya awali na jukumu lisilobadilika kwa Kituo kikuu cha Radio na Televisheni. Mwaka 2019 ni mwaka wa Maadhimisho ya miaka 70 tangu Jamhuri ya watu wa China ianzishwe, ambapo Kituo kikuu cha Radio na Televisheni cha taifa cha China kitafanya juhudi zaidi kuwaelezea wasikilizaji na marafiki zetu popote walipo kuhusu hali halisi ya China kwa pande zote katika Zama mpya.

    Marafiki zetu wapendwa:

    Wakati tunapokaribisha Mwaka mpya, kwa niaba ya Kituo kikuu cha Radio na Televisheni cha taifa cha China na wenzangu wote, ninamtakia kila msikilizaji wetu furaha ya mwaka mpya na kila la kheri.

    Katika miaka 1300 iliyopita, mshairi mashuhuri wa Enzi ya Tang ya China Wang Boi alipoagana na rafiki yake aliandika shairi lisemalo, "Marafiki wa dhati wapo popote duniani, lakini mioyo yao daima inakuwa karibu", nikinukuu shairi lake, naona linaweza kueleza vilivyo hisia zangu za sasa kwa marafiki zetu wapendwa.

    Hivi sasa labda kwako wewe msikilizaji wetu, unayosikia ni sauti mpya, kwani Mwezi Machi mwaka jana, ili kufuata mwelekeo wa maendeleo ya vyombo vya habari duniani, Kituo kikuu cha Radio na Televisheni cha taifa cha China kiliundwa kwenye msingi wa Radio China Kimataifa CRI, Kituo cha taifa cha televisheni CCTV na Radio ya Serikali kuu ya China CNR.

    Tunawashukuru marafiki zetu mapya na wa tangu zamani ambao wametutia moyo kwa udhati, hatutasahau nia yetu ya awali na jukumu letu siku zote! Kituo Kikuu cha Radio na televisheni cha taifa cha China kilichoundwa upya, kingali bado kinabeba jukumu lake la kutoa habari za nchini China kwa dunia, kutangaza habari za dunia kwa China, na kuhimiza maelewano na urafiki kati ya watu wa nchi mbalimbali duniani. Ni matumaini yetu kuwa tutafanya kazi vizuri zaidi na kuwahudumia zaidi!

    Rais Xi Jinping alisema: "Maendeleo ya China hayawezi kutengana na dunia, na ustawi na neema ya dunia pia vinaihitaji China." Katika mwaka uliopita tulitumia kamera, microphone na kalamu zetu kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano na maelewano kati ya China na dunia.

    Matangazo yetu kuhusu Maadhimisho ya miaka 40 tangu China ianze kufanya mageuzi na kufungua mlango, kuhusu Maonesho ya kwanza ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, na Baraza la Ushirikiano wa China na Afrika yalifuatiliwa na wasikilizaji wetu wengi; tulishikilia msimamo wetu wa kithabiti ulio wazi, tukitoa sauti ya kutetea usawa na haki kuhusu kulinda biashara huria na kuhimiza mafungamano ya uchumi duniani, tena tulitoa sauti ya China kwenye Mkutano wa wakuu wa APEC, Mkutano wa Wakuu wa G20, hayo yote yametambuliwa na wasikilizaji wetu popote walipo; tumejitahidi kutumia lugha za nchi mbalimbali kuhusisha vyombo vya habari vya China na nchi mbalimbali kama vile Russia, Italia, Japan, Hispania na nyinginezo, ili wasikilizaji wetu wapate habari nyingi zaidi, shughuli mbalimbali za "kupongeza Jumuiya la Ushirikiano la Shanghai", "Kukutana kwenye Maonesho ya Kwanza ya kimataifa ya Bidhaa ziagizwazo kutoka nje" ziliwavutia mashabiki wengi wa nchi mbalimbali; tumefanya juhudi za kuwasiliana na dunia, na kutangaza "Mkutano wa kilele wa vyombo vya habari vya Asia kwenye Baraza la Asia la Boao", na "Baraza la Hongqiao la kimataifa la vyombo vya habari za mambo ya fedha na uchumi na Jumuiya ya washauri bingwa", hayo yote yalifuatiliwa na vyombo vingi vya habari wa dunia, na shughuli kuhusu "Maonesho ya filamu za China barani Afrika" , "Maonesho ya michezo ya sanaa ya China", na "Mimi ni shabiki wa China" zimewafanya marafiki zetu wengi wanaipende China na kuwa mashabiki wa China.

    Katika mwaka mpya, tutafanya Maadhimisho ya miaka 70 ya Jamhuri ya Watu wa China. Kituo kikuu cha Radio na televisheni cha taifa cha China kitafanya juhudi kubwa zaidi ili kuwaelezea marafiki zetu hali ya China kwa pande zote katika Zama mpya.

    Katika mwaka mpya, tutawaletea marafiki zetu vipindi vingi vizuri vitakavyowavutia zaidi, kuwashangaza zaidi na kuwawezesha mvipende zaidi, ambapo tutaeleza ukweli wa mambo ili kuonesha hali halisi ya China ambayo ni "mjenzi wa amani ya dunia, mchangia maendeleo ya dunia nzima na mlinzi wa utaratibu wa kimataifa"

    Tutafanya juhudi za kuvumbua mbinu mpya za matangazo, kutumia ipasavyo teknolojia mpya za 5G, AI, Big Data na Hesabu za mawingu, ili kuharakisha maendeleo yenye sifa bora na ya kuruka ngazi, kuchapa kazi zaidi kujenga kituo chetu cha radio na televisheni kiwe cha aina mpya cha kiwango cha juu dunia, ili kukuhudumia vizuri zaidi wewe msikilizaji wetu.

    Rafiki yetu wa tangu zamani Yury Tavrovsky ambaye ni mtaalamu maarufu wa Elimu ya Lugha ya Kichina wa nchi ya Russia, alitunga kitabu cha "Xi Jinping: Anayetimiza Ndoto ya China", alikuwa ametupigia simu akisema: "Nina imani thabiti kuwa pendekezo la China kuhusu kujenga Jumuiya ya mustakabali wa pamoja ya binadamu, ni Taa ya kuangaza mwelekeo wa njia ya maendeleo ya dunia". Aliyosema ni kweli, binadamu wote sisi tuna sayari moja ya dunia, nchi mbalimbali zinaishi pamoja kwenye dunia moja. Tufanye juhudi kwa pamoja ili kujenga jumuiya ya mustakabali ya pamoja ya binadamu, kujenga dunia yenye amani ya kudumu, usalama popote tulipo, ustawi na neema za pamoja, kufungua mlango wazi na kufanya ushirikiano wa pande nyingi na yenye usafi na uzuri!

    Nikutakia tena kila la kheri! Asante sana !   

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako