• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China awapongeza viongozi wa Cuba kuadhimisha miaka 60 ya ushindi wa mapinduzi

    (GMT+08:00) 2019-01-01 17:54:30

    Rais Xi Jinping wa China kwa niaba ya Chama cha Kikomunisti cha China na watu wa China, mapema leo ametuma salamu za pongezi kwa katibu wa chama cha Kikomunisti cha Cuba Raul Castro pamoja na rais Miguel Diaz-Canel wa Cuba kuadhimisha miaka 60 ya ushindi wa mapinduzi wa nchi hiyo.

    Katika ujumbe wake kwa viongozi hao, rais Xi amesema chini ya uongozi thabiti wa Chama cha Kikomunisti cha Cuba kwa miaka 60 iliyopita, serikali ya Cuba na watu wake wamepiga hatua kubwa ya kimaendeleo pamoja na kufanya kazi kwa bidii kutokana na ujenzi wa ujamaa.

    Vilevile rais Xi ameeleza China itaendelea kushirikiana na Cuba kuleta maendeleo ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako