• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uagizaji sukari kutoka mataifa nje uliongezeka msimu wa sherehe

  (GMT+08:00) 2019-01-01 18:20:05
  Uagizaji wa sukari kutoka mataifa ya nje uliongezeka kwa asilimia 107 mwezi wa kumi na moja mwaka 2018, nchini Kenya. Hii ni kufuatia shamra shamra za sikuku ya Krismasi na sherehe za mwaka mpya zilizowalazimisha wauzaji wa bidhaa hii kuagiza kutoka nje. Kulingana na takwimu, takriban tani 39, 752 za sukari ziliingizwa nchini mwaka wa 2018, huku tani 17,917 zikiagizwa mwezi wa Novemba. Uzalishaji wa sukari kutoka kwa kampuni za Kenya ulikuwa tani 38, 768. Kwa pamoja, uzalishaji wa sukari kuanzia mwezi Januari hadi Novemba mwaka uliopita, ulikuwa tani 450,335, ukilinganishwa na tani 327,211 kipindi sawia na hicho mwaka wa 2017. Ikumbukwe kwamaba mwezi Mei mwaka uliopita, serikali ya Kenya ilitupilia mbali utozaji ushuru kwa sukari kutoka mataifa ya nje baada ya uhaba wa sukari humu nchini, uliosababishwa na kiangazi kilichoathiri ukulima wa miwa. Uganda imekuwa ikiuza sukari yake kwa mataifa mengine kutokana na uzalishaji bora uliopo kwenye taifa hilo.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako