• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Riadha: Wakenya watawala mbio za San Silvestre nchini Uhispania

  (GMT+08:00) 2019-01-02 09:05:29

  Wakenya Brigid Kosgei na Hellen Obiri wamenyakua nafasi mbili za kwanza kwenye mbio za kilomita 10 za San Silvestre nchini Uhispania mnamo Desemba 31, 2018. Kosgei, ambaye alishinda taji la Chicago Marathon mwezi Oktoba mwaka 2018, alinyakua ubingwa wake wa pili wa San Silvestre Vallecana baada ya mwaka 2016 kwa kuweka rekodi mpya ya dakika 29:54. Alifuta rekodi ya Muethiopia Gelete Burka ya dakika 30:53 iliyowekwa mwaka 2012. Muethiopia Tirunesh Dibaba, ambaye alikuwa amepigiwa upatu kubeba taji, aliridhika katika nafasi ya tatu kwa dakika 30:40. Nafasi tatu za kwanza za wanaume zilinyakuliwa na Mganda Jacob Kiplimo (dakika 26:41), Muethiopia Abadi Hadis (26:54) na Mganda Mashe Bushendich (27:24), mtawalia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako